29 Mei 2026 - 18:46
Mafuriko Makubwa ya Mto Furati Yatikisa Syria; Maelfu ya Familia Wakosa Makazi

Kufunguliwa kwa milango ya Bwawa la Atatürk nchini Uturuki kumesababisha mafuriko makubwa katika maeneo ya Deir ez-Zor na Raqqa nchini Syria, huku zaidi ya hekta 24,000 za mashamba zikiharibiwa na maelfu ya wananchi kulazimika kuhama makazi yao.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- maeneo makubwa ya vijijini katika mikoa ya Deir ez-Zor na Raqqa nchini Syria yamekumbwa na mafuriko makubwa kufuatia kufunguliwa kwa milango ya Bwawa la Atatürk nchini Uturuki, jambo lililosababisha kuongezeka kwa kiwango cha maji katika Mto Furati kwa kiwango kisichokuwa cha kawaida.
 
Mafuriko hayo yamezizamisha maelfu ya hekta za mashamba ya ngano yaliyokuwa katika hatua za mwisho za kuvunwa, hali iliyoongeza hofu ya kuongezeka kwa uhaba wa chakula na kudorora kwa maisha ya wakulima katika maeneo yaliyoathirika.
 
Aidha, vituo muhimu vya usambazaji maji ya kunywa pamoja na miundombinu ya huduma za kijamii vimeripotiwa kuharibika vibaya kutokana na nguvu ya maji hayo, huku baadhi ya miji na vijiji vikiendelea kuzingirwa na mafuriko.
 
Janga hilo pia limewalazimu maelfu ya familia za Syria kuhama makazi yao na kukimbilia katika vituo vya muda vya hifadhi, ambapo wanakabiliwa na changamoto kubwa za maisha kutokana na uhaba wa huduma muhimu na misaada ya kibinadamu.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, takribani hekta 24,000 za ardhi ya kilimo zimeharibiwa hadi sasa, wakati juhudi za misaada zikielezwa kuwa bado ni ndogo mno ukilinganisha na ukubwa wa maafa yanayoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha